Muwakilishi wa mawakibu Husseiniyya katika mji wa Basra amesema: Zaidi ya maukubu (1970) zinashiriki kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Muwakilishi wa mawakibu Husseiniyya katika mkoa wa Basra chini ya kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, amesema kuwa jumla ya mawakibu zinazo shiriki kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini mwaka huu ni zaidi ya (1970) zilizo sajiliwa kwenye orodha ya kitengo cha mawakibu.

Kwa mujibu wa maelezo ya bwana Mundhir Hamiid Nizaal, akaongeza kuwa: “Zinaingia chini ya uwakilishi wetu idara ishirini, sita ndani ya mkoa na kumi na nne zimegawanywa katika idara za mkoa, zipo hadi sehemu za mbali kabisa na mkoa kama vile Fau, kutokana na kufungamana kwake na mikoa mingine ya kusini, mawakibu hizo zimejipanga katika barabara zinazo tumiwa na mazuwaru wengi, sambamba na kuyapa kipaombele maeneo yenye mazuwaru wengi”.

Akafafanua kuwa: “Kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya janga la Korona, maukibu zote zimechukua tahadhari kwa kutekeleza maagizo yote ya idara ya afya kuhusu njia za kujikinga na maambukizi, kama vile kupuliza dawa, kuvaa barakoa pamoja na kutumia vifungashio katika kugawa chakula, bila kusahau kufuata masharti ya afya wakati wa kuandaa chakula, hali kadhalika tunatembelea mawakibu na kuangalia kama zinatekeleza kikamilifu masharti yote yaliyo tolewa na idara ya afya”.

Akabainisha kuwa: “Mwaka huu harakati za mazuwaru zimeanza mapema, misafara ya watu wanaokwenda Karbala ilianza kupita mapema, nazo maukibu za kutoa huduma ya chakula na matibabu hazikubaki nyuma, zimekua mstari wa mbele katika kutoa huduma na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya misafara ya mazuwaru kuisha hapa mkoani ndio watumishi wa mawakibu hizo wataanza safari ya kutembea kwenda Karbala, ili wapate utukufu mara mbili, wa kutoa huduma na kufanya ziara”.

Kumbuka kuwa uliwekwa mkakati maalum ulio husisha wadau wote wa utoaji wa huduma, ambao ni askari, madaktari na wawakilishi wa mawakibu, na wote wanafanya kazi kwa bidii ili kufanikisha ziara hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: