Kamati ya maandalizi ya kongamano la kielimu kuhusu Imamu Hassan (a.s) chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya kitengo cha makongamano ya kielimu na kitamaduni hapa Iraq

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano inafanya kongamano la saba la Imamu Hassan Almujtaba (a.s), ambalo limeanza asubuhi ya Ijumaa mwezi (7 Safar 1442h) sawa na tarehe (25 Septemba 2020m), Atabatu Abbasiyya tukufu ni mlezi mkuu wa harakati za kielimu na kitafiti, imekua ikifadhili makongamano ya kielimu na kitamaduni kwa manufaa ya taifa letu kipenzi.

Hayo yamesemwa katika ujumbe wa ufunguzi ulio tolewa na Dokta Sarhani Jaffaat kwaniaba ya kamati, miongoni mwa aliyo sema ni: “Kwa mara nyingine tumekutana katika ukumbi wa Abu Muhammad Hassan Almujtaba (a.s) na ni mara nyingine tumekutana na kalamu tukufu za kielimu zilizo pambwa na mapenzi ya Muhammad na Aali Muhammad (a.s), pamoja na mapenzi ya elimu iliyo jengewa kwenye msingi madhubuti, kongamano hili la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ambalo ni kongamano la saba linalo fanywa katika mazingira ya janga la Korona, janga ambalo limesababisha kusimama kwa shuguli nyingi za kibinaadamu, lakini halijaweza kusimamisha shughuli za kielimu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Makongamano ya kielimu yanapewa kipaombele sana na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, wakati wote Mheshimiwa amekua mstari wa mbele katika kusaidia tafiti za kielimu na kufadhili makongamano mbalimbali kwa maslahi ya taifa letu kipenzi, tunatoa pongezi kwa kila atakae shiriki kwenye kongamano hili chini ya kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu).

Akamaliza kwa kusema: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ajalie mambo yatakayo fanywa katika kongamano hili yawapandishe daraja mbele yake (s.w.t) na mbele ya watu wa nyumba ya Mtume watoharifu, na tunaishukuru sana idara ya elimu na ubunifu pamoja na kituo cha Al-Ameed Duwaliyyu Lilbuhuthi wa Dirasaat, bila kuisahai kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan (a.s), Tunamuomba Mwenyezi Mungu awawezeshe na awape taufiq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: