Kuanza awamu ya saba ya kongamano la kielimu kuhusu Imamu Hassan Almujtaba (a.s)

Maoni katika picha
Kwa ufadhili wa uongozi mkuu wa Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya na kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan (a.s), pamoja na kushirikiana na vyuo viwili cha Alkafeel na Al-Ameed na kituo cha Al-Ameed, shughuli za kongamano la saba kuhusu Imamu Hassan Almujtaba (a.s) zimeanza asubuhi ya Ijumaa mwezi (7 Safar 1442h) sawa na tarehe (25 Septemba 2020m), chini ya anuani asemayo: (Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika historia tukufu ya Mtume) linalo fanywa kupitia jukwaa la (zoom).

Kongamano lilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Sayyid Hasanaini Halo, baada ya Quráni ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu (Lahnul-Ibaa), kisha ukatolewa ujumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili, ulio wasilishwa na Dokta Sarhani Jaffaat, akabainisha kuwa: Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu ni mlezi mkubwa wa harakati za kielimu na kitafiti, imekua ikifadhili shughuli mbalimbali za kielimu kwa maslahi ya taifa letu kipenzi.

Halafu ikafuata mada ya ufunguzi iliyo wasilishwa na Dokta Abdulhasan Jaduu Abdul-Abudi kutoka chuo kikuu cha Kufa/ kitivo cha malezi ya msingi, mada ilikuwa inasema (Athari ya Imamu Hassan katika kuhuisha sunna za Mtume), kisha ukafunguliwa mlango wa majadiliano na maswali, ambapo mtoa mada alijibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale alipo takiwa kufanya hivyo, mada za kitafiti zitaendelea kuwasilishwa saa tisa mchana baada ya Adhuhuri hii leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: