Hospitali ya rufaa Alkafeel imekamilisha maandalizi ya kushiriki katika kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini mkoani Karbala

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel kila mwaka huandaa mkakati wa kutoa huduma za afya kwa mazuwaru wa Arubaini mkoani Karbala, kwa kujenga vibanda vya kutolea huduma ya afya na kuweka madaktari wa maradhi tofauti na wauguzi kwa ajili ya kutibu mazuwaru.

Hospitali imetangaza kuwa imekamilisha maandalizi yote ya kutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru, mkuu wa kitengo cha habari katika hospitali ya Alkafeel amesema kuwa: “Hii sio mara ya kwanza kushiriki hospitali kwenye mkakati wa kutoa huduma ya afya katika ziara wa Arubaini, ilishiriki katika ziara nne za mwisho zilizopita”.

Akaongeza kuwa: “Hospitali inamchango mkubwa katika kutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru katika ziara zote zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.

Akasema: “Jukumu la vibanda vya afya vinavyo jengwa ni kutoa matibabu kwa mazuwaru na kuangalia hali ya mgonjwa kama sio nzuri hupelekwa kwenye hospitali ya karibu”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hutoa matibabu kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa chini ya madaktari mahiri kutoka ndani na nje ya nchi. Kila baada ya muda fulani hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa ambao wapo katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: