Muhimu: Ziara ya Arubaini kwa niaba ya kila aliyeshindwa kuja mwaka huu

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa wito kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kote duniani, wale walioshindwa kuja katika ardhi ya kujitolea, ardhi ya Twafu, kufanya ziara ya Arubaini katika mazingira haya ya uwepo wa janga la virusi vya Korona, wasajili majina yao kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba ufuatao https://alkafeel.net/zyara/.

Kiongozi wa idara ya taaluma na mitandao chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir, amesema: “Huduma ya ziara kwa niaba inatolewa na ukurasa huo kwenye mtandao wa Alkafeel, huchukua jukumu la kufanya ziara maalum kwa niaba, ikiwemo ziara ya Arubaini, mwaka huu tumeipa kipaombele zaidi kutokana na idadi kubwa ya watu kutoka ndani na nje ya Iraq kushindwa kuja kufanya ziara kwa sababu ya janga la virusi vya Korona, janga ambalo limepelekea kufungwa mipaka kwa ajili ya kujilinda na virusi hivyo”.

Akaongeza kuwa: “Tumefungua milango ya usajili mapema kupitia dirisha la ziara kwa niaba, siku kumi kabla ya ziara, ili kutoa nafasi ya kusajili watu wengi zaidi, kupitia mitandao yote iliyo chini ya toghuti yetu pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii, jopo la masayyid wanaofanya kazi Atabatu Abbasiyya watafanya ziara hizo kwa niaba ya waliojisajili”.

Akabainisha kuwa: Ibada ya ziara ya Arubaini itafanywa ndani ya haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na swala ya ziara na dua kwa watu wote walio jisajili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: