Vituo vya Ashura: Mjumbe wa mfalme wa Roma akumbatia kichwa kitakatifu kifuani kwake na atangaza kuingia katika uislamu, na Yazidi aamuru auwawe.

Maoni katika picha
Imepokewa kutoka kwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s) anasema: Kilipo letwa kichwa cha Hussein (a.s) kwa Yazidi, alikua akikaa kunywa pombe anaagiza aletewe kichwa cha Hussein (a.s) na anakiweka mbele yake, siku moja akaingia mjumbe kutoka kwa mfalme wa Roma, alikua ni miongoni mwa watu watukufu wa Roma, akasema: ewe mfalme wa waarabu, hiki kichwa cha nani? Yazidi akamuambia: hauna haja ya kichwa hiki. Akasema: Nikirudi kwa mfalme wangu ataniuliza kila kitu nilicho ona, nitapenda kumuambia kisa cha kichwa hiki na mwenye nacho, ili aungane na wewe katika shangwe na furaha. Yazidi akamuambia: Hiki ni kichwa cha Hussein mtoto wa Ali mtoto wa Abu Twalib. Akasema: Mama yake ni nani? Akasema: Fatuma Zaharaa mtoto wa Muhammad Mustwafa!!.

Yule mkristo akasema: hauoni ninapo muangalia muili wangu unasisimka, na ninamsikia anasoma aya za kitabu chenu!. Ushindwe wewe na dini yako, dini yangu ni bora kuliko dini yako. Tambua kua baba yangu anatokana na vitukuu vya Daudi (a.s), kati yangu na yeye kuna vizazi vingi, lakini wakristo wananitukuza kiasi huchukua mchanga wa nyayo zangu na kutabaruku, na nyie mnauwa mtoto wa mtoto wa Mtume wenu (s.a.w.w) ambae baina yake na Mtume wenu ni mama mmoja tu?! Dini yenu ni ya aina gani? Kana kwamba hamjamuamini Mtume wenu hadi mmemfanyia namna hii.

Katika kitabu cha (Almufidu katika kumbukumbu ya mjukuu shahidi) cha Sayyid Abdulhussein Ibrahim Aamili kimeandika kua: yazidi hakupata cha kumjibu yule mnaswara, akasema kwa ujinga na jeuri: kama isingenifikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kua atakae uwa mtu asiye na hatia atakua adui wake siku ya kiyama ningekuuwa kwa sababu ya maneno yako, mkristo akasema: Ajabu iliyoje kwa ujinga wako ewe Yazidi!. Mtume atakua vitu adui wa mtu atakae uwa mtu asiye na hatia halafu asiwe adui wa aliye uwa watoto wake na wajukuu wake?

Yazidi akachukia na akasema: Muuweni huyu mnaswara asiende kutufedhehesha kwenye mji wake.

Alipo hisi kuwa anauwawa, alimuuliza: Unataka kuniuwa? Akasema: Ndio.. lazima nikuuwe. Akasujudu juu ya ardhi kumshukuru Mwenyezi Mungu, na akasema: tambua kuwa usiku wa leo nilimuona Mtume wenu katika usingizi, akaniambia: Ewe mkristo, wewe ni katika watu wa peponi. Nilishangaa sana maneno hayo.

Kisha akakumbatia kichwa cha Imamu Hussein (a.s) na akakiweka kifuani kwake, akakibusu na kulia, akasema: Amani iwe juu yako ewe Abu Abdillahi Hussein na rehema zake na baraka zake, nitolee ushahidi mbele ya Mola wako na babu yako na baba yako na mama yako na kaka yako, kuwa mimi: nashuhudia hakuna Mungu ispokua Allah mmoja asiyekua na mshirika, na ninashuhudia kuwa hakika Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Ali ni walii wa Mwenyezi Mungu.

Wakamkata panga na kumuuwa, rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: