Wawakilishi wa mawakibu za Muthanna wamesema: Zaidi ya maukibu (1850) zimeshiriki kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Wawakilishi wa mawakibu chini ya kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili takatifu wamesema kuwa: “Mawakibu zilizo shiriki kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini ndani ya mipaka ya mkoa wa Muthanna ni zaidi ya (1850) zilizo sajiliwa rasmi na kitengo cha mawakibu, miongoni mwa hizo zipo (290) zitatoa pia huduma katika mkoa wa Karbala, bado kuna mamia ya Husseiniyya na nyumba za makazi pamoja na maukibu ambazo hazikujisajili na zimefungua milango yao na kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru tangu siku ya kwanza ambayo mazuwaru wameanza kuingia katika mji huu, tena kuanzia kwenye mpaka wa mkoa huu na mwingine”.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa wawakilishi wa maukibu bwana Saádi Abdaliyyu, akaongeza kusema kuwa: “Mwaka huu maandalizi ya maukibu zilizo vuka mpaka hadi kwenye mkoa wa Dhiqaar hadi mkoa wa Qadisiyya yalianza mapema, maukibu hizo zimeenea kwenye barabara zote zinazo tumiwa na mazuwaru, katika maeneo ya mji hadi maeneo ya jangwani, mwaka huu tulijenga sehemu za kutolea huduma za afya pamoja na gari zilizo kuwa zinatembea na kutoa huduma hiyo, sambamba na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akabainisha kuwa: “Mwaka huu harakati za mazuwaru zilianza mapema, mawakibu za kutoa huduma jukumu lake halikuishia kwenye kuhudumia mazuwaru peke yake, bali zimetoa ushirikiano mkubwa sana kwa vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mji huu, wahudumu wa mawakibu wataenda Karbala kufanya ziara na kupata utukufu mara mbili, wa kutoa huduma kwa mazuwaru na kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: