Kiongozi mkuu wa maendeleo ya viwanda amesema kuwa: Miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni ya kisasa na inatoknolojia kubwa imesaidia kurudisha neno (Imetengenezwa Iraq)

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa maendeleo ya viwanda na kilimo kutoka wizara ya viwnanda ya Iraq Mhandisi Raaid Abdu-Ilaaha Aljaburi amesema kuwa: “Miradi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ni ya kisasa na inateknolojia kubwa, imechangia kuongoza ajira na kupunguza tatizo la ukosefu wa kazi”.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya, kama vile shirika la biashara Alkafeel na baadhi ya viwanda vilivyo chini yake, pamoja na Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji na kituo cha maegesho Alkafeel.

Akaongeza kusema kuwa: “Hakika miradi hii inasifa kubwa ya kutegemea uwezo wa raia wa Iraq, na inafanya kazi kulingana na mazingira halisi, imesaidia kurudisha sentesi isemayo (Imetengenezwa Iraq), vyombo vya habari vya ndani vinatakiwa kutangaza miradi hii, yenye faida kubwa mkowani Karbala na Iraq kwa ujumla”.

Ugeni huo ulifuatana na kiongozi mfawidhi wa shirika la Alkafeel, Mhandisi Rasulu Abduridhwa Ramahi ambaye amesema kuwa: “Leo tumetembelewa na mkuu wa idara ya maendeleo ya viwanda, amekuja kuangalia miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, amesikiliza maelezo kwa ufupi kuhusu kila mradi, yaliyo tolewa na wasimamizi wa miradi hiyo, ilikuwa nafasi nzuri kwa idara ya widara kuangalia miradi inayo fanywa hapa nchini, na kwa namna gani ndani ya muda mfupi imeweza kuwa alama kubwa ya viwanda. Ugeni umepongeza miradi hiyo na huduma zake muhimu kwani imeongeza uzalishaji wa taifa na kupunguza uagizaji wa bidhaa nje ya nchi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: