Vituo vya Ashura: Yazidi aruhusu mateka watoke jela na akusudia kumuua Imamu Zainul-Aabidina

Maoni katika picha
Fadhili Darbandi anasema: Sababu zilizo pelekea Yazidi kuiachia familia ya Mtume (s.a.w.w) kutoka jela, aliona miujiza ya wazi kwenye kichwa kitakasifu na kwa watu wa familia ya Mtume (s.a.w.w), ilimtokea mara nyingi.

Miongoni mwa miujiza huo, ni ndoto ya kutisha aliyo ota katika usiku ambao mke wake Hindu aliota pia, kauli ya Hindi inaonyesha jambo hilo, anasema: “Nikaanza kumtafuta Yazidi mara nikamkuta ameingia kwenye nyumba ya giza akiwa uso wake umeangalia ukutani, huku anasema: Nina nini mie kumuua Hussein…)

Miongoni mwake: Ndoto aliyo ota mke wake Hindu.

Miongoni mwake: Ndoto aliyo ota kijakazi, aliona kundi la malaika wanataka kuchoma nyumba ya Yazidi na kila kilichomo.

Miongoni mwake: Ndoto ya Sukaina (a.s) na kisa chake, ambacho tumesha kitaja.

Mambo hayo yalisababisha hofu katika moyo wa yule kafiri, aliogopa kuanguka utawala wake na yeye kufa, hakika sababu kubwa roho yake ilijaa hofu na uoga, kwa sababu ya maneno yaliyokua yanasemwa na watu kuhusu yeye, na watu wa Sham kuanza kuwa dhidi yake, na kuanza kudhaniwa kuwa inawezekana wakamvamia.

Siku aliyo waacha huru kutoka jela, Yazidi alimwita Imamu Zainul-Aabidina (a.s), alikua anataka aongee ili amuuwe, Mwenyezi Mungu akamzuwia.

Alama Majlisi katika kitabu cha Albiharu anasema: Imepokewa kuwa Imamu Zainul-Aabidina alipo pelekwa kwa Yazidi akiwa anataka kumuua, alisimamishwa mbele yake, akaanza kumuambia maneno ya kumtaka aongee ili apate sababu ya kumuuwa, Ali bun Hussein (a.s) akawa anamjibu kama anavyo ulizwa, huku mkononi mwake (a.s) akiwa na tasbihi ndogo anamjibu huku anaizungusha, Yazidi akamuambia: Mimi nakuongelesha na wewe unanijibu huku unazungusha tasbihi!. Nani kakuruhusu kufanya hivyo?

Akasema (a.s): Aliniambia baba yangu kutoka kwa babu yangu, alikua anaposwali Subhi haongei bila kuwa na tasbihi mkononi kwake, anasema: Ewe Mola mimi nimeamka nikiwa nakusabihi na kukusifu, nasoma tahlili na takbira na kukutukuza, kwa idadi ninayo zungusha tasbihi yangu. Huku anazungusha tasbihi mkononi mwake, na anaongea anacho taka kwa tasbihi, akasema hiyo ndio suna yake, na ndio hirzi yake hadi atakaporudi kitandani, na akilala anasema kama alivyo sema asubuhi, kisha anaweka tasbihi chini ya kichwa chake, alikua anafanya hivi kila wakati, mimi nimefanya kumuiga babu yangu.

Yazidi akasema: Kwa mara nyingine, siongei na yeyote katika nyie ispokua atanipa majibu ya kumfanya afaulu na nimsamehe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: