Mawakibu za kuomboleza (zanjiil) zinahuisha utiifu kwa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Malalo mbili takatifu ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), asubuhi ya mwezi (16 Safar 1442h) sawa na tarehe (4 Oktoba 2020m) mawakibu za kuomboleza (zanjiil) zimeanza kumiminika kwenye malalo hizo moja baada ya nyingine, kutoka mikoa tofauti ya Iraq kama ilivyo pangwa kwenye ratiba, na kuanza ukurasa mpya wa uombolezaji wa Arubaini, zitaendelea kwa muda wa siku mbili, wanamaukibu wanaingia wakiwa wanapiga vifua vyao na kutokwa machozi kwa uchungu wa tukio la Twafu, wanampa pole Imamu wa zama (a.f) na kuhuisha utiifu wao kwa bwana wa mashahidi (a.s).

Hayo yanafanywa chini ya utekelezaji mkubwa wa kanuni za afya kwa wanamaukibu na wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wanafuata maelekezo yote yaliyo tolewa na idara ya afya na kuhimizwa na Marjaa Dini mkuu, ikiwa ni pamoja na kuheshimu umbali kati ya mtu na mtu, kuvaa barakoa na soksi za mikononi, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyadh Niímah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ratiba ya mawakibu za (zanjiil) ni sehemu ya uombolezaji katika msimu wa Arubaini, maukibu hizo zinaanzia matembezi yake katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi kwenye haram yake takatifu, wanaimba kaswida zinazo onyesha maumivu ya roho zao kutokana na kumbukumbu ya Arubaini ya bwana wa vijana wa peponi (a.s), kisha wanaenda katika haram ya ndugu yake shujaa wa Twafu na mbeba bendera wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili hadi kwenye kaburi la bwana wa maji, wanapo fika hapo huangua kilio kikubwa kwa mara nyingine na huimba tenzi za kuomboleza msiba huu mkubwa katika umma wa kiislamu”.

Kumbuka kuwa mawakibu ya zanjiil watu husimama mistari miwili mirefu na hutembea kwa pamoja, katikati yao huwa kuna vijana walioshika bendera, huku unapikwa mdundo kwa sauti na waomolezaji hupandisha zanjiil na kujipiga mgongoni kwa kufuata mdundo, mazuwaru husimama pembezi ya barabara na kuangalia matembezi ya mawakibu huseiniyya, vitendo hivyo huongeza Imani na mapenzi kwa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: