Idara ya uhusiano wa vyuo vikuu na shule imevipa vituo vya kuelekeza mazuwaru Zaidi ya wanafunzi wa chuo (300).

Maoni katika picha
Idara ya uhusiano wa vyuo na shule chini ya kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imevipa vituo vya kuelekeza mazuwaru na kusaidia waliopotea au kupotelewa Zaidi ya wanafunzi (300) kutoka vyoo vikuu na maahadi za Iraq, baada ya idara ya mawasiliano na teknolojia katika kitengo cha miradi ya Ataba takatifu kuandaa vifaa vyote vinavyo hitajika kiufundi na kiteknolojia.

Ustadh Muntadhwiru Swafi kiongozi wa idara ya harakati za vyuo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni mwaka wa kumi mfululizo idara yetu inavipa vituo hivi wanafunzi wa vyuo na maahadi, walioshiriki miaka ya nyuma na wapya, wanaoshiriki kwa mara ya kwanza baada ya kupewa mafunzo maalum ya uendeshaji wa vituo hivyo, na hufanya kazi saa (24) kwa siku katika zamu tatu”.

Akaongeza kuwa: “Wanafunzi wamesambazwa kwenye vituo (45) vilivyopo katika barabara zinazo elekea Karbala, upande wa Baabil, Bagdad, Najafu pamoja na ndani ya mji wa Karbala ambo una vituo sita, katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu na kwenye maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) na jengo la Husseini katika barabara ya Jamhuriyyah, pamoja na kwenye eneo la mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akafafanua kuwa: “Wanafunzi hao kazi zao haziishii katika vituo hivyo peke yake, wapo wanaofanya kazi katika vituo vya ukaguzi pia ambavyo vimeunganishwa na vituo hivyo kwa njia ya kielektronik, na wapo wanaofanya kazi ya kupeleka mtu aliyepotea kwenye vituo vya kupumzikia watu hao vilivyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu hadi watakapo kutana na jamaa zao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: