Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari vinavyo penda kutangaza matukio ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari vinavyo penda kutangaza matukio ya ziara ya Arubaini, wanatakiwa kuwasiliana na uongozi wa kitengo hicho kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kisheria, ikiwa ni pamoja na kuwarahisishia uingiaji katika Ataba mbili na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kwa kuwapa vitambulisho maalum kutokana na kazi yao.

Hayo yamesemwa na makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Ahmadi Swadiq, akaongeza kuwa: “Kwa ajili ya kuratibu utangazaji wa habari za ziara ya Arubaini katika picha sahihi, na kuondoa migongano kati ya kitengo cha habari na waandishi wa habari, kitengo kimeweka utaratibu maalum kwa vyombo vya habari, kila muandishi wa habari anatakiwa kuwa na kitambulisho kinacho onyesha jina la chombo cha habari, jina lake na aina ya kazi yake (luninga – gazeti – redio na vinginevyo) pamoja na orodha kamili ya waandishi wa habari anao fanyanao kazi, kisha wanapewa kitambulisho (baji) itakayo warahisishia utendaji wao chini ya kanuni tulizo kubaliana”.

Akamaliza kwa kusema: “Kitengo kitatoa maelekezo maalum kwa waandishi wa habari wanaopenda kutangaza matukio ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na yatatangazwa hivi karibuni”.

Akasisitiza ulazima wa kuheshimu maelekezo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: