Kitengo cha usimamizi wa haram tukufu kunachukua hatua za kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya kazi kubwa ya kupuliza dawa katika haram takatifu, kwa ajili ya kulinda usalama wa mazuwaru na mawakibu za waombolezaji katika kipindi hiki cha ziara ya Arubaini, na kuweka mazingira salama kiafya kama ilivyo elekezwa na idara ya afya.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi amesema kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu wanaheshimu na kufanyia kazi maelekezo yaliyo tolewa na idara ya afya, wanapuliza dawa katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye milango yake muda wote sambamba na kwenye mabusati, aidha kuna vijana wanaopuliza dawa mawakibu na kwenye vituo vya ukaguzi”.

Akaongeza kuwa: “Pamoja na tuliyo taja, wanapuliza dawa pia kwenye sardabu na sehemu zilizo ongezwa pamoja na sehemu za kubumzika mazuwaru, kwa kutumia vifaa maalum, na tenki za dawa za kubeba mgongoni pamoja na mitungi ya gesi”.

Kumbuka kuwa kazi hii ni sehemu ya mkakati wa kiutumishi katika Atabatu Abbasiyya, ulio anza kutekelezwa tangu siku za kwanza kuingia mazuwaru wa Arubaini, maandalizi yalifanywa mapema kwa namna ambayo inalinda afya na usalama wa mazuwaru na watumishi kwa pamoja, katika mazingira magumu ya ziara hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: