Namna gani utamlinda mtoto wako asipotee katika ziara ya Arubaini?

Maoni katika picha
Kamati inayo husika na kuongoza waliopotea na waliopotelewa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefafanua njia ambayo mtu anaweza kupata alicho poteza au mtu aliye potea, kwa kuripoti kwenye kituo cha karibu yake kinacho husika na kuongoza walio potea, vituo hivyo vipo maeneo tofauti pembezoni mwa mji wa Karbala, upande wa mkoa wa Baabil, Najafu na Bagdad, pamoja na ndani ya mji mtukufu wa Karbala, kuna jumla ya vituo (45).

Msimamizi mkuu wa kitengo hicho Ustadh Muntadhir Swadiq kiongozi wa idara ya harakati za vyuo amesema kuwa: “Idara ya mawasiliano na teknolojia chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa vifaa vyote vinavyo hitajika katika kazi hiyo, na vinaongozwa na wataalamu kutoka vyuo vikuu na Maahadi za Iraq, ambao wanafanya kazi kwa kujitolea baada ya kuwasiliana na idara ya uhusiano wa vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya kazi usiku na mchana, wamepewa simu za kuwasiliana kati ya kituo na kituo, pamoja na mawasiliano ya redio coll”.

Akaongeza kuwa: “Kuhusu zana zinazo saidia kupata kitu kilicho potea au mtu aliye potea, ni mfumo maalum uliowekwa kwenye vituo hivyo unaofanya kazi kupitia ukurasa wa maelezo, unao ingizwa maelezo ya kila aliyepotea, (jina, umri, anuani na mengineyo), baada ya kuingiza maelezo hayo huonekana moja kwa moja kwenye vituo vyote”.

Akabainisha kuwa: “Kila mtu anaweza kuona taarifa hizo kupitia screen iliyo wekwa juu ya mlango wa kila kituo, aidha wanatumia pia vipaza sauti kutangaza walio potea na kuna gari maalum za kuwabeba na kuwapeleka kwa jamaa zao, vituo hivyo vinashirikiana na sekta zingine za Atabatu Abbasiyya, na vimeunganishwa na makao makuu ya ukaguzi”.

Kuwasiliana na kituo cha kusaidia walio potea au kupotelewa piga namba zifuatazo muda wowote ndani ya saa (24).

-07602405909

-07602421330

-07706730387

-07706730407
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: