Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimetoa ratiba ya uingiaji wa mawakibu za matam

Maoni katika picha
Baada ya kuisha siku mbili za kuingia mawakibu za zanjiil, kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chuni ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimetoa ratiba maalum ya mawakibu za matam zinazo shiriki katika Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu, ambazo pia zitaingia kwa muda wa siku mbili, hadi mwezi kumi na tisa Safar.

Rais wa kitengo hicho Bwana Riyadh Ni’mah Salmaan amesema kuwa: “Viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kutoka mikoa yote ya Iraq wanatakiwa kuheshimu ratiba hiyo, tambua kuwa ratiba hiyo inaanzia muda wa kuondoka katika jukwaa lililopo karibu na maonyesho ya barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s), hadi kuingia katika Atabatu Husseiniyya tukufu kisha kuelekea katika Atabatu Abbasiyya na kumaliza matembezi yao hapo, tunatarajia kuheshimiwa ratiba tuliyotaja kwa ajili ya kumtumikia Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru wake watukufu”.

Akasisitiza kuwa: “Ni lazima kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi na kufuata maelekezo ya kitengo cha maadhimisho na mawakibu kwa kuzingatia ratiba ya kila mkoa kama ilivyo tangazwa”.

Ratiba yenyewe ni:

Safar 18

Mkoa wa Naswiriyya na vitongoji vyake kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.

Mkoa wa Ammaarah na vitongoji vyake kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 Adhuhuri.

Maukibu ya kuomboleza ya baraza kuu na taasisi ya Badri kuanzia saa 7 Adhuhuri hadi saa 8 baada ya Adhuhuri.

Mkoa wa Diyala na Swalahu Dini kuanzia saa 8 baada ya Adhuhuri hadi saa 10 Alasiri.

Kikundi cha Answari Shahidi Swadri kuanzia saa 10 Alasiri hadi saa 11:30 jioni.

Mkoa wa Waasit na vitongoji vyake kuanzia saa 1 usiku hadi saa 2 usiku.

Mkoa wa Diwaniyya na vitongoji vyake kuanzia saa 2 usiku hadi saa 4 usiku.

Mkoa wa Bagdad na vitongoji vyake kuanzia saa 4 usiku hadi saa 5 usiku.

Mawakibu kutoka nchi za kiarabu na kiislamu kuanzia saa 5 usiku hadi saa 6 usiku.



Safar 19

Kadhimiyya takatifu kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 2 asubuhi.

Moka wa Najafu na vitongoji vyake kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.

Mkoa wa Basra na vitongoji vyake kuanzia saa 7 baada ya Adhuhuri hadi saa 8 baada ya Adhuhuri.

Maukibu ya Hizbu-Da’wah na kabila la Bani Tamimi kuanzia saa 10 Alasiri hadi saa 11:30 jioni.

Mkoa wa Karkuuk na Nainawa kuanzia saa 1 jioni hadi saa 3 usiku.

Wilaya ya Ainu-Tamru kuanzia saa 3 usiku hadi saa 4 usiku.

Mawakibu kutoka nchi za kiarabu na kiislamu kuanzia saa 4 usiku hadi saa 6 usiku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: