Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Muhammad Asadi amesema kuwa, maelekezo hayo ni:
- - Kuzingatia sehemu na muda uliopangwa kupiga picha.
- - Kutoa ushirikiano na idara za Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kulinda utukufu wa ziara.
- - Atakae poteza kitambulisho au akachelewa kukabidhi atalipa faini ya dinari (250,000).
- - Idara za Ataba mbili tukufu zinahaki ya kukagua kamera kabla na baada ya kupiga picha na zinahaki ya kufuta chochote zitakacho ona kinafaa kufutwa.
- - Hairuhusiwi kufanya mahojiano ya mubashara au yasiyokua mubashara bila kujua idara za Ataba mbili tukufu.
- - Hairuhusiwi kutoa kitambulisho nje ya eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, lazima urudishe kitambulisho baada ya kumaliza kupiga picha.
- - Muandishi wa habari anatakiwa akabidhi kitambulisho chake cha uraia na cha chombo cha habari anacho fanyia kazi.
- - Hairuhusiwi kupiga picha binafsi ndani ya maeneo tuliyo taja.