Hospitali ya Alkafeel inatoa huduma za matibabu mfululizo kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa huduma za matibabu kwa mazuwaru wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kupitia vibanda vya afya ilivyo jenga pamoja na kwenye jengo lake la hospitali.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya habari katika hospitali hiyo Ustadh Twariq Twarafi, akaoneza kuwa: “Hospitali ya Alkafeel kwenye msimu wa ziara hii imeweka utaratibu maalum wa utowaji wa huduma za afya kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona”,

Utoaji wa huduma umegawanyika sehemu mbili ambazo ni:

Kwanza: Tumefungua vituo viwili vya utoaji wa huduma za afya, cha kwanza katika barabara ya Najafu/ Karbala, na cha pili karibu na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), vituo hivyo vinaendeshwa na madaktari na wauguzi wenye ujuzi na uzowefu mkubwa wa kukabiliana na hali yeyote atakayo kuanayo mgonjwa, pamoja na kutoa huduma za kujikinga na maambukizi, kama vile kugawa barakoa na baadhi ya vitu muhimu kwa mazuwaru.

Pili: Hospitali imeandaa gari maalum za wagonjwa kwa ajili ya kubeba wale watakao hitaji kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi, gari hizo zina madaktari na wauguzi wenye uwezo wa kupambana na hali yeyote ya maradhi atakayo kuanayo mgonjwa”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika vituo vyetu vya afya vilianza kazi tangu misafara ya mazuwaru ilipoanza kuingia Karbala mwezi kumi Saraf, na vitaendelea kutoa huduma hadi baada ya msimu wa ziara ya Arubaini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: