Wahudumu wa kitengo cha utumishi wameanza kazi ya kusafisha maeneo yote yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Wahudumu wa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi, kama kawaida yao baada ya msimu wa ziara ya Arubaini kila mwaka, hufanya usafi katika maeneo yote yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya pamoja na kwenye barabara zinazo elekea Ataba na ndani ya mji mkongwe, huondoa kila aina ya uchafu.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Muhammad Ahmadi Jawadi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa idara yetu wameanza kazi ya usafi mapema leo asubuhi, wanasafisha barabara zote zinazo zunguka na kuelekea Atabatu Abbasiyya sanjari na kuzisafisha kwa maji (kupiga deki) kwa kutumia gari maalum”.

Akaongeza kuwa: “Aidha wamepiga deki na kusafisha tabaka la chini katika Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kuongoka watu waliokua wanajitolea kuhudumia mazuwaru, wameondoa mazulia yote yaliyokua yametandikwa na kuyapeleka stoo, halafu wametandika mazulia mapya, kabla ya kutandika mazulia hayo walipiga deki”.

Akasema: “Kazi ya usafi imehusisha pia ukumbi wa Aljuud uliopo upande wa barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumefanya usafi pia katika njia za maji”.

Akamaliza kwa kusema: “Bado tunaendelea na kazi hiyo, tutasafisha pia barabara zingine, kadri mazuwaru wanavyo pungua na sisi tunaongeza wigo wa kazi”.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo ambavyo humuhudumia moja kwa moja zaairu, nacho hufanya kila kiwezalo kutoa huduma bora zaidi katika ziara tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: