Kwa upasuaji wa aina yake: Uondoaji wa mifuko kwenye moyo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka (16) katika hospitali ya rufaa Alkafeel

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumfanyia upasuaji mgonjwa aliyekua na tatizo la kuziba kwa mirija na kuwa na mifuko kwenye moyo wake.

Daktari aliyeshiriki kwenye upasuaji huo Dokta Muayyad Naqiib amesema kuwa: “Mgonjwa mwenye umri wa miaka (16) alikua na tatizo la kuziba mirija kwa zaidi ya mwezi, kwa sababu ya kuwa na mifuko ya maji kwenye moyo wake, tumefanikiwa kumtibu katika hatua tatu”.

Akaongeza: “Baada ya kufanyiwa vipimo kwa kina ikagundulika kuwepo kwa mifuko kwenye moyo inayo sababisha kuziba mirija ya damu”.

Akaendelea kusema: “Ndipo mgonjwa akapelekwa kwenye jopo la madaktari bingwa waliomuwekea kifaa cha kuzuwia kuziba, na kurudisha ujendaji wa moyo katika hali ya kawaida katika hatua ya kwanza”.

Akasema: “Katika hatua ya pili akafanyiwa matibabu maalum ya kuondoa maji katika mifuko hiyo kidogo kidogo kwa muda wa mwezi mmoja na nusu, kisha tukaingia katika hatua ya tatu na ya mwisho ambayo amefanyiwa upasuaji na kuondoa mifuko ya maji pamoja na kurekebisha sehemu zilizo kua zimeathirika”.

Tambua kuwa: “Baada ya kufanyiwa matibabu ya hatua ya tatu kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa, mgonjwa amepona kabisa”.

Tunapenda kusema kuwa Hospitali ya rufaa Alkafeel, hutoa huduma bora wakati wote kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel, hupokea madaktari bingwa wa maradhi tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa ambao wapo katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: