Idara ya stoo: Imefanya kazi kubwa ya kujenga hema za watumishi wa kujitolea katika shule zilizo teuliwa kuwahifadhi wakati wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya stoo imefanya kazi kubwa ya kujenga hema za kukaa watumishi wa kujitolea katika shule zilizo teuliwa kuwahifadhi wakati wa ziara ya Arubaini..

Idara ya stoo chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kazi kubwa ya kukarbati shule zilizo tunza wafanyakazi wa kujitolea, waliokuja Karbala kuwahudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka mikoa tofauti ya Iraq.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Haidari Abbasi Hussein ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa idara yetu walifanya matengenezo katika shule saba, zilizo tunza wafanyakazi wa kujitolea waliokuja kuhudumia mazuwaru wakati wa ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa: “Tulishirikiana na kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi kufanya matengenezo katika vyoo vya shule hizo na kuweka mazingira vizuri ya kukaa wafanyakazi wa kujitolea, sambamba na kujenga hema na mabanda ya kulala wakati wote waliokua Karbala na kuweka mahitaji yote muhimu”.

Akaendelea kusema: “Baada ya kumaliza ziara tumeanza kusafisha shule hizo na kuzikabidhi kwa idara ya malezi ya Karbala”.

Kuhusu vitakasa mikono na barakoa amesema kuwa: “Tuliongeza juhudi ya kugawa barakoa na vitakasa mikono, kama sehemu ya kukidhi mahitaji ya Ataba tukufu kuhusu vifaa hivyo, ukizingatia kuwa ugawaji wa vifaa hivyo unachukuliwa kuwa jambo muhimu sana”.

Kumbuka kuwa idara ya stoo ipo chini ya kitengo cha utumishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: