Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa salam za rambirambi kufuatia msiba wa mhadhiri wa mimbari Husseiniyya Sayyid Jaasim Towirajawi (Mwenyezi Mungu amuweka katika rehema zake)

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa salam za rambirambi kwa kufiwa na mhadhiri wa Twafu, Sayyid Towirajawi, aliyefikwa na umauti Alfajiri ya leo Jumapili (22 Safar 1442h) sawa na tarehe (11 Agosti 2020m) baada ya kuugua, tamko la rambirambi linasema:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatuma salam za rambirambi kwa huzuni kubwa na majonzi, kufuatia kifo cha mhadhiri wa mimbari Husseiniyya Sayyid Jaasim Towirajawi, aliye tumia umri wake mtukufu katika njia ya kutumikia mimbari ya Husseiniyya na kusariri nchi hadi nchi katika njia hiyo, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amuweke katita rehema zake na amfufue pamoja na babu yake Imamu Hussein (a.s), aipe familia yake na wapenzi wake subira na uvumilivu..

Hakuna hila wala nguvu ispokua ni kwa Mwenyezi Mungu Mkuu Mtukufu
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: