Miongoni mwa mfululizo wa mkakati wa maarifa: Toleo la juzuu la kwanza na la pili katika kundi la vitabu vya (Sisi na mambo ya mwanamke)

Maoni katika picha
Kituo cha Uislamu na utafiti wa kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa juzuu la kwanza na la pili katika mfululizo wa machapisho ya vitabu vya (sisi na mambo ya mwanamke) chini ya mkakati wa maarifa, siku za nyuma walitoa kitabu cha (sisi na magharibi.. ukaribu wa mihadhara ya Imani ya kiislamu – sisi na turathi zetu kimaadili – sisi na zama za ukoloni – sisi na malezi ya kiislamu), kituo bado kinaendelea kuchapisha vitabu katika mfumo huo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyo tolewa na mkuu wa kituo hicho Sayyid Hashim Milani, amesema kuwa: Hakika hizi juzuu mbili zimetokana na kazi ya jopo la watafiti, na kuhaririwa na Dokta Muhsin Mussawi pamoja na Ustadh Ali Muhammad, inahesabika ni sehemu ya kufikia ramani ya maarifa ya kiislamu katika mambo yanayo husu mwanamke, kwa namna ambayo inaendana na uhalisia pamoja na mazingira ya zama hizi, kupitia mfumo huo ndio unabainishwa wajibu wa mwanamke na mwanaume, bila kujali yanayo fundishwa na nchi za magharibi pamoja na vikundi vya haki za binaadamu vinavyo tokana na tamaduni zingine.

Akaongeza kuwa: “Uandishi wa vitabu hivyo umehusisha jopo la watafiti, ili kubainisha nafasi ya mwanamke katika uislamu haki zake na wajibu wake, pamoja na kujibu maswali yote yaliyotolewa na wanaharakati wa wanawake, kunahaja ya kulipa umuhimu mkubwa swala hili, bali kuanzisha kituo kitakacho shughulikia swala hili”.

Mwisho Sayyid Milani akaelekeza shukrani zake kwa kila aliyechangia katika kufanikisha uandishi wa vitabu hivi, kuanzia watafiti, wahariri, wafasiri na wasanifu waliofanya kazi kubwa hadi wakafanikisha kutolewa kwa vitabu hivi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: