Kitabu cha (Karbala katika mashairi ya Lebanon) kinaonyesha urithi wa washairi (38) wa kilebanon jinsi walivyo athiriwa na Karbala

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinajitahidi kufichua yaliyo andikwa kuhusu tukio la Twafu, hususan mashairi yanayo husu tukio hilo kubwa, na sasa kimekuja kitabu cha (Karbala katika washairi wa Lebanon) ni moja ya vitabu vilivyo tolewa na kituo chini ya utaratibu huu.

Kitabu kina kurasa (310) nacho kimeandikwa na raia wa Lebanon, ametumia utaratibu unaofanana na utaratibu wa tafiti, kwa kufanya mahojiano na washairi wa zama hizi, au kurejea mashairi ambayo watunzi wake hawako hai, kimetaja kwa ufupi kuhusu kila mshairi na mashairi yake yanayo husu harakati tukufu ya Husseiniyya na Karbala, pamoja na maelezo kuhusu madhumuni ya beti hizo.

Ndio kikatolewa kitabu chenye utangulizi wa kituo cha turathi za Karbala, kisha kikatolewa na Sayyid Hussein Sharafu-Dini Al-Aamiliy -mkuu wa kituo cha Imamu Abdul-Hussein Sharafu-Dini Al-Aamiliy- halafu kuna utangulizi wa muandishi, kisha muna matini iliyo andikwa na muandishi ambayo ametaja washairi (38), kwa kufuata mpangilio wa herufu katika kuandika majina yao, ambapo alikua anakusudua kuangalia turathi za washairi wa Lebanon, na namna wanavyo lichukulia tukio la Twafu.

Kitabu kimetaja baadhi ya kauli za Mustashriqina kuhusu Imamu Hussein (a.s) na Karbala, kituo cha turathi za Karbala kikakamilisha kurasa za mwisho kwa kuandika rejea za vitabu na faharasi pamoja na mambo ya kitaaluma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: