Wingu la huzuni limetanda katika Atabatu Abbasiyya kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Maoni katika picha
Wingu la huzuni na majonzi limeongezeka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hali hiyo ilianza tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam, katika kumbukumbu ya tukio la Twafu na kilele chake kufikiwa katika siku hizi, hakika limeongezeka kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Mtume wa rehema na muombezi wa umma Muhammad bun Abdillahi (s.a.w.w), aliyetumwa na Mwenyezi Mungu mtukufu kuwa muokozi wa walimwengu, akamfanya kuwa muongoaji, mkumbushaji na nuru, aidha akamfanya kuwa mfikishaji wa ujumbe wake, kila sehemu ya ataba inaonyesha ujumbe wa huzuni na majonzi kutokana na kumbukumbu ya masiba mkubwa katika umma wa kiislamu unaosadifu mwezi (28 Safar 1442h).

Yamewekwa mapambo yanayo ashiria huzuni kwenye mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kwenye milango mingine ya haram tukufu, kama tangazo la kuanza msimu wa huzuni za Muhammadiyyu na kwenye sehemu zingine ndani na nje wa harama takatifu.

Kumbuka kuwa kifo cha Mtume wa mwisho Muhammad bun Abdillah (s.a.w.w) kilitokea mwezi (28) Safar mwaka wa (11) hijiriyya, akiwa na umri wa miaka (63), wafuasi na wapenzi wake katika mnasaba huu, huelekea katika kaburi la simba wa Mwenyezi Mungu mwenye kushinda Ali bun Abu Twalib (a.s) kumpa pole kufuatia kifo cha ndugu yake mtoto wa Ammi yake Mtume wa rehema Muhammad (s.a.w.w), nayo ni katika ziara maalum, asilimia kubwa ya mazuwaru baada ya kumaliza ziara hiyo huelekea Karbala, kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: