Mwezi ishirini na nane Safar ni kumbukumbu ya msiba wa uislamu kifo cha muongoaji wa binaadamu Mtume wa rehema (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo (28 Safar) mwaka wa 11 hijiriyya umma wa kiislamu ulipata msiba wa kuondokewa na Mtume mtukufu, Mtume wa rehema na muombezi wa umma Muhammad bun Abdillahi (s.a.w.w), aliyeletwa na Mwenyezi Mungu kuwa muokozi wa binaadamu, na akamteuwa kuwa muongoaji, muonyaji na nuru kwa walimwengu wote, akampa jukumu la kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu.

Imepokewa kutoka kwa Imamu Muhammad Baaqir (a.s) anasema: “Ulipofika wakati wa kifo cha Mtume (s.a.w.w), alikuja Jibrilu (a.s) akasema: Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu unataka kurudi duniani na umesha fikisha? Akasema: hapana, kisha akamuambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unataka kurudi duniani? Akasema: hapana, nataka kwenda kwa Mwenyezi Mungu”.

Alifariki Mtume (s.a.w.w) mkono wa kulia wa kiongozi wa waumini (a.s) ukiwa chini ya shavu lake, Mtume (s.a.w.w) alikua ameshasema: Nitaoshwa na mtu wa karibu yangu zaidi, na kulikua hakuna mtu wa karibu yake zaidi ya Ali (a.s), Imamu Ali alipo maliza kumuosha Mtume (s.a.w.w), alifunua shuka usoni kwake (s.a.w.w) akasema huku anatokwa machozi:

Kwa haki ya baba na mama ulikua mzuri ulipokua hai na upo mzuri baada ya kifo, kifo chako kimekata mambo ambayo hayakukatika kwa kifo cha asiyekua wewe, umekatika utume na unabii. Lau usingeamrisha subira na ukakataza kutokuwa na subira, tungemaliza juu yako maji mengi na yangekua tiba, lakini usichoweza kukirudisha hauwezi kukitoa, kwa haki ya baba na mama tukumbuke mbele ya Mola wako, na utuweke katika akili yako.

Kisha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) alikuwa mtu wa kwanza kumswalia Mtume (s.a.w.w), halafu waislamu wakamswalia makundi kwa makundu, na akazikwa ndani ya chumba chake.

Wakati wa mwisho wa uhai wake (s.a.w.w) hakua na watu wengine zaidi ya Ali bun Abu Twalib na bani Hashim na wanawake wao, watu wakafahamu kifo chake (s.a.w.w) kutokana na sauti za kilio zilizo sikika katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w) kufuatia kifo chake, nyoyo zilihuzunika sana kwa kuondokewa na mbora wa viumbe wa Mwenyezi Mungu. Habari ya kufa kwake ikaenea katika mji wa Madina kwa haraka, huzuni na majonzi vikaenea kwa kila mtu pamoja ya kua Mtume (s.a.w.w) alikua amesha andaa mazingira ya kifo chake, aliongea kuhusu kifo chake mara nyingi, akahusia umma mambo ya muhimu ikiwa ni pamoja na kumtii khalifa wake baada yake ambaye ni Ali bun Abu Twalib. Hakika kifo chake kilikua pigo kubwa kwa wauslamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: