Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume wa mwisho

Maoni katika picha
Asubuhi ya Ijumaa mwezi ishirini na nane Safar 1442h, Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) chini ya usimamizi wa idara ya masayyid katika Ataba tukufu ndani ya ukumbi wa Aljuud (mkabala na mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi –a.s-), sambamba na kufuata masharti yote ya afya yaliyo husiwa na Marjaa Dini mkuu pamoja na wizara ya afya.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Ataba tukufu, Sayyid Hashim Shami amesema kuwa: “Majlisi ya kuomboleza itafanywa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo, chini ya uhadhiri wa Shekh Haidari Hamidawi na kuhudhuriwa na watumishi wa malalo pamoja na mazuwaru watukufu kama sehemu itakavyo ruhusu, kwa kuzingatia kujiepusha na msongamano na kufuata maelekezo ya mamlaka za afya”.

Akasema: “Mhadhiri ataeleza utukufu wa Mtume (s.a.w.w) katika upande wa tabia na ubinaadamu wake (s.a.w.w), ukizingatia kuwa ujumbe wa Muhammad ndio ujumbe mkubwa kutoka mbinguni ulio shuhudwa hapa duniani, kisha majlisi zitafungwa kwa kuimba tenzi za kuomboleza”.

Akamaliza kwa kusema: “Kila mwaka hufanywa majlisi kama hii ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), lakini kutokana na mazingira ya mwaka huu, ya janga la virusi vya Korona, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu kwa baraka za huyu tunae mkumbuka, akuondolee balaa hili, tumelazimika kufanya majlisi katika sehemu hii ambayo kitengo cha utumishi kimechukua jukumu la kufanya usafu na kupuliza dawa pamoja na kuweka viti kwa kuzingatia umbali kati ya mtu na mtu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: