Mawakibu za ustawi wa jamii zinahitimisha huduma zake kwa kuwahudumia mazuwaru wa kiongozi wa waumini (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa imehitimisha shughuli zake kwa kuhudumia mazuwaru wa kiongozi wa waumini (a.s), waliokuja katika malalo yake takatifu kumpa pole kwa kifo cha ndugu yake na mtoto wa Ammi yake Mtume Muhammad (s.a.w.w), kupitia uwepo wa idadi kubwa ya mawakibu zinazo fungamana na idara hiyo kwenye mikoa tofauti.

Kiongozi wa idara bwana Qassim Ma’muri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kushiriki zaidi ya maukibu (500) katika miji tofauti ya Iraq chini ya mkakati uliowekwa na idara ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya, wa kuhudumia mazuwaru wa Arubaini waliokuja katika ardhi ya watu huru kutoka kila sehemu, na kumaliza huduma hizo kwa mafanikio makubwa, ambapo huduma ilikuwa inatolewa saa 24 kila siku katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya mji wa Karbala, na katika barabara zinazo elekea Karbala, sasahivi watumishi wa maukibu hizo wameelekea Najafu kuhudumia mazuwaru wa kiongozi wa waumini (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Mawakibu zinatoa huduma tofauti ikiwa ni pamoja na kugawa barakoa kwa mazuwaru na waombolezaji wanao fanya majlisi za Husseiniyya, sambamba na kuheshimu masharti ya afya ikiwa ni pamoja na kuheshimu umbali kati ya mtu na mtu, shughuli hizi zinahitimisha kazi yetu katika msimu huu wa maombolezo, tutaendelea kutoa huduma za kibinaadamu pamoja na kusaidia jeshi la serikali na wapiganaji wa Hashdu-Shaábi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: