Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake imesema kuwa: Mamia ya mazuwaru wa kike wametembelea hema za Abulfadhil Abbasi (a.s) kujifunza usomaji sahihi wa surat Fat-ha

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imesema kuwa mamia ya mazuwaru wa kike wamenufaika na huduma ya usomaji wa Quráni iliyo tolewa na Maahadi, kupitia mradi wa ufundishaji wa Quráni katika hema la Abulfadhil Abbasi (a.s), wamefundishwa usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na sura pufu.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika Maahadi hufanya shughuli mbalimbali wakati wa ziara ya Arubaini, hujenga mabanda ya kufundishia usomaji sahihi wa Quráni katika barabara zinazo tumiwa na mazuwaru wanaotembea kwenda Karbala, kutokana na janga la virusi vya Korona, mwaka huu tumefanya baadhi ya mambo, ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Hema za Quráni zilikua na majukumu mengi, miongoni mwa majukumu hayo ni kusikiliza usomaji wa surat Fat-ha na kusahihisha makosa katika usomaji wa sura hiyo, sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona wakati wa kusikiliza na kufundisha usomaji sahihi wa Quráni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: