Idara ya wanawake imetoa huduma katika jengo la Alqami

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya wamejitolea kuhudumia mazuwaru katika jengo la Alqami lililopo barabara ya (Karbala – Baabil), wametoa huduma mbalimbali zinazo endana na mazingira ya mwaka huu ya uwepo wa maambukizi ya virusi vya Korona.

Kiongozi wa kituo hicho bibi Firdausi Ali Hasuun ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumefanya kazi kubwa inayo endana na mazingira ya uwepo wa maambukizi ya virusi vya Korona, yanayo hitaji kuwa na maandalizi maalum, kama vile kuandaa dawa za kupuliza pamoja na vitu vingine vya kujikinga na maambukizi vinavyo hitajiwa na zaairu mtukufu”.

Akaongeza kuwa: “Mwaka huu tumekuwa na utaratibu maalum katika kuandaa sehemu za kupumzika na kulala, ulio zingatia umbali kati ya mtu na mtu na kupuliza dawa kwenye matandiko kila wakati, pamoja na kusambaza vipeperushi vya maelekezo ya kujikinga na maambukizi kwa mazuwaru”.

Akafafanua kuwa: “Hali kadhalika tumegawa barakoa na vitakasa mikono kwa watoa huduma pamoja na sare maalum kwa wale wanaotoa huduma katika sehemu za vyoo”.

Kumbuka kuwa watumishi na wahudumu wa kike katika Ataba tukufu na wale wanaojitolea kuhudumia mazuwaru, wamezowea kutoa huduma kila mwaka katika kituo hiki na vinginevyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: