Mamia ya sahani za chakula zimetolewa na mgahawa wa mwenye ukarim (Swahibul-Juud) kwa mazuwaru ndani ya siku mbili

Maoni katika picha
Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) umegawa mamia ya sahani za chakula ndani ya siku mbili mfululizo, katika ziara ya kukumbuka kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupitia madirisha yake ya nje na kwa kuzingatia tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, ili kulinda usalama wa mazuwaru na watumishi wa mgahawa.

Rais wa kitengo cha mgahawa Mhandisi Aadil Hamami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mgahawa wa Atabatu Abbasyya tukufu umetoa huduma ya chakula kwa mazuwaru walio kuja Karbala kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Ndani ya siku mbili mfululizo, wale ambao hawakuweza kwenda katika mji wa Najafu kuomboleza msiba huo”.

Akaongeza kuwa: “Kama kawaida ugawaji wa chakula umefanywa kwa mpangilio mzuri kupitia mistari miwili, wa wanaume na wanawake”.

Akaendelea kusema: “Tulichukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi kama tulivyo fanya katika ziara ya Arubaini, tumegawa chakula kupitia vyombo vya plastiki vya kutumika mara moja, na watoa huduma wote walikua wamevaa barakoa na soksi za mikononi”.

Kumbuka kuwa mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu hutoa huduma ya chakula kwa mazuwaru kila siku, ni kielelezo kikubwa cha ukarimu wa Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: