Kuanza awamu ya tano ya kongamano la kimataifa Al-Amiid

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo (Tunakutana katika ukumbi wa Al-Ameed kwa maendeleo) na kwa anuani ya (Selibasi ya kufundishia na tafiti.. kuithibitisha, kuihalili na kuiandaa), kituo cha kimataifa cha utafiti Al-Ameed chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Alkhamisi (4 Safar 1442h) sawa na tarehe (22 Oktoba 2020m), kimeanza awamu ya tano ya kielimu na kimataifa Al-Ameed kwa kushirikiana na jumuiya ya Al-Ameed na chuo kikuu cha Alkafeel na Al-Ameed, kongamano hili litadumu kwa muda wa siku tatu kupitia jukwaa la (zoom).

Kongamano limepata muitikio mkubwa, watu kutoka nchi (14) za kiarabu na kiajemi wanashiriki, bila kusahau taifa mwenyeji la Iraq, limefunguliwa kwa Quráni tukufu, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa la Iraq na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa), ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Halafu ukafuata ujumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano, ulio wasilishwa na Dokta Abbasi Rashidi Mussawi, akafafanua kuwa tayali amesha pitia mihtasari ya mada za washiriki zaidi ya mia moja, na tafiti hamsini na nne, katika hizo zimechaguliwa tafiti thelathini, tano katika hizo; zitawasilishwa katika kongamano kwa lugha ya kiengereza.

Kisha itaonyeshwa filamu ya kongamano pamoja na mafanikio yaliyo patokana katika awamu zilizo pita, hadi kufikia awamu hii ambayo kongamano linafanywa katika mazingira ya pekee.

Baada ya hapo ikawasilishwa tafiti ya ufunguzi na Ustadh Ahmadi Ali Muhammad Atwiyya, iliyokuwa inasema: (Uhakika wa selebasi katika ufundishaji – kwa mfano nadhariya ya kanuni za lugha).

Tambua kuwa kongamano litakua na vikao vinne vya mada za kitafiti kutoka kwa wasomi wa ndani na nje ya Iraq, zitakazo tolewa kupitia link ifuatayo:

https://us02web.zoom.us/j/3740873005

Meeting ID: 374 087 3005
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: