Waziri wa umeme amesema kuwa: Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kazi kubwa katika kuboresha uwezo wa umeme hapa mkoani Karbala na tunatarajia uhusiano utaimarika zaidi

Maoni katika picha
Waziri wa umeme Mhandisi Majidi Mahadi amesema kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kazi kubwa katika kuboresha umeme wa mkoa wa Karbala, na sisi kama wizara tunatarajia kuimarisha uhusiano zaidi. Ameyasema hayo alipotembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), alipokelewa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, akasikiliza maelezo ya hatua muhimu zilizo chukuliwa na Ataba tukufu katika kuongeza uwezo wa umeme, pamoja na utumiaji wa umeme mbadala katika miradi yake mingi, kabla ya hapo alitembelea kituo cha umeme cha Alkafeel ambacho ujenzi wake umefika zaidi ya asilimia %98 kitakacho zalisha kilobait 11/33, utakao maliza tatizo la umeme katika eneo lote la kusini mwa Karbala.

Akafafanua kuwa: “Leo tumetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na tumepata nafasi ya kutoa shukrani kwa kujenga vituo vinne vya umeme katika mkoa wa Karbala, ushirikiano unaendelea kati ya wizara na Ataba tukufu, tunatarajia wataendelea kujenga vituo zaidi, tutafanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha mkoa unapata umeme wa uhakika mwaka kesho kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: