Kiongozi mkuu wa kisheria ametembelea kituo cha uchapishaji na usambazaji Darul-Kafeel.

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea kituo cha uchapishaji na usambazaji Darul-Kafeel kukagua mitambo ya kisasa iliyo fungwa na kituo hicho, kwa ajili ya kuongeza uwezo wa uchapishaji na kuacha kutegemea nje ya taifa sambamba na kuhuisha neno lisemalo (Kimechapishwa Iraq).

Tumeongea na mkuu wa kitengo hicho Mhandisi Farasi Ibrahim kuhusu ziara hiyo amesema kuwa: “Tumetembelewa na Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekagua kazi ya mwisho tuliyo fanya ambapo tumeongeza uwezo wa uchapishaji”.

Akaongeza kuwa: “Hivi karibuni tumeongeza mitambo mipya, ambayo imeongeza uwezo wa uchapaji hadi kufikia karatasi elfu thelethini kwa saa katika kila mtambo, sambamba na kuweka mtambo mwingine wa hati kutoka Ujerumani na mtambo wa majalada kutoka Uswisi”.

Akasisitiza kuwa: “Tunalenga kusaidia juhudi za wizara ya malezi pamoja na taasisi zingine, kwa kuchapisha kiwango kikubwa cha vitabu na kulinda mali kwa kuizungusha ndani ya nchi, sambamba na kupunguza tatizo la upungufu wa ajira ikiwa ni pamoja na kuhuisha neno lisemalo (kimechapishwa Iraq) na kusaidia harakati za uandishi katika jamii”.

Akamaliza kwa kusema: “Sisi tunafuata mkakati wetu wa maendeleo ya uchapaji tulio jiwekea hadi mwaka 2030m”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: