Mwezi tano Rabiul-Awwal alifariki mtu anaefanana sana na bibi yake Zaharaa bibi Sakina (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi mtukufu wa Rabiul-Awwal unamambo mengi ya kihistoria yaliyotokea katika umma wa kiislamu, miongoni mwa mambo hayo ni hili la tarehe tano katika mwezi huu mwaka wa (117h), siku hiyo alifariki bibi Sakina mtoto wa Imamu Hussein (a.s) na kipenzi chake.

Bibi Sakina (a.s) ni Amina bint Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s), mama yake ni Rubabu bint Amri Alqais bun Adi Alkalbiy, amekua mashuhuri kwa jina la (Sakina) kutokana na utulivu, upole na unyenyekevu, alikuwepo katika tukio la Twafu huko Karbala, aliona kwa macho yake mauwaji makubwa, kuuwawa kwa baba yake Imamu Hussein (a.s), watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, alikumbatia muili wa baba yake baada ya kuuwawa kwake, na alichukuliwa mateka pamoja na watu wengine wa familia ya Mtume (a.s), wakatembezwa kutoka Karbala hadi Kufa wakiwa na watu waliobeba vichwa vya mashahidi, kisha wakatolewa Kufa wadi Sham, na baada ya hapo alirudi Madina pamoja na kaka yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s) na mateka wengine.

Riwaya zinaonyesha kuwa alizaliwa (a.s) mwaka wa arubaini na saba hijiriyya, wakati wa kuuwawa baba yake Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala alikuwa na umri wa miaka kumi na nne, miaka yote hiyo aliimaliza akiwa chini ya malezi na uangalizi wa baba yake bwana wa mashahidi (a.s), kupata malezi ya moja kwa moja kutoka kwa mtakasifu kulimjenga sana kielimu, kidini na kimaadili, pamoja na kuathiriwa na familia ambayo imejaa watu watakasifu, hakika alikuwa na kiwango cha juu cha elimu, maarifa na uchamungu.

Baada ya tukio la Twafu na yaliyo endelea kujiri alishiriki na alipambana kwa ajili ya Mola wake, aliuthibitishia ulimwengu kuwa na msimamo na uimara wa idikadi, bibi Sakina (a.s) aliendelea kuwa chini ya usimamizi wa Imamu Sajjaad (a.s), maisha yake yalijaa elimu adabu na harakati za kijamii, hata wapinzani wake walisifu nasabu na maadili yake.

Bibi Sakina alikua mbora wa wanawake wa zama zake, alikua muelewa zaidi, mwenye akili ya hali ya juu, mwenye adabu njema, mwenye kujitunza, vikao vya wanawake wa Madina vilikuwa vinapambwa kwa elimu, adabu na uchamungu wake, alikuwa mfasaha, baba yake Imamu Hussein (a.s) anathibitisha uchamungu wake na namna alivyokua akiswali swala za usiku, anasema: (Amma kwa hakika Sakina amezama katika kumuabudu Mwenyezi Mungu), aliyasema hayo pale alipotaka kuposwa na Hassan mtoto wa Hassan mtoto wa Ammi yake (a.s), akamchagulia dada yake Fatuma.

Alifariki (a.s) mwezi tano Rabiul-Awwal mwaka wa 117h katika mji wa Madina, akazikwa katika makaburi ya Baqiii, kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Shadharaat-Dhahabu na akanukuu Sayyid Muhsin Amiin katika kitabu cha Aáyaani, alifariki katika mji wa Madina siku ya Alkhamisi mwezi tano Rabiul-Awwal mwaka wa 117h, ni mashuhuri kuwa alizikwa Madina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: