Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimechangia kuhuisha maktaba ya Allamah Ayatullahi Sayyid Hassan Swadr (q.s)

Maoni katika picha
Kutokana na umuhimu wa kuhakiki na faharasi katika kutunza turathi za umma na kuziendeleza kwa vizazi vijavyo, idara ya kutunza maarifa chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imechapisha kitabu cha (Kubaini tunu za maktaba ya Abu Muhammad Hassan).

Kitabu hicho ni faharasi ya maktaba ya Allamah Ayatullahi Sayyid Hassan Swadr aliyekufa mwaka (1354h), kilicho kusanywa na mtoto wake Allamah Sayyid Ali bun Sayyid Hassan Swadr Alkadhwimiy aliyekufa mwaka (1380h), na kikahakikiwa na Mheshimiwa Sayyid Jafari Husseiniy Ashkuriy.

Kitabu hicho kimewekwa katika ngazi ya wizara, na majina ya vitabu yameandikwa kwa kufuata mpangilio wa herufi, kuna jumla ya vitabu (561).

Makamo rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu Mheshimiwa Shekh Ali Asadiy, amesema kuwa: “Tangu kuanzishwa kwa kitengo hiki, kimekuwa kikifanya uhakiki wa turathi za kiislamu, kutokana na umuhimu wake na kuzilinda zisipotee na kusahaulika, ukizingatia kuwa umuhimu wa kila umma unapatikana katika turathi zake na historia yake, kwani turathi huonyesha nafasi waliyo kuwa nayo”.

Akasema: “Mafanikio haya ni sehemu ya vitabu vilivyo tutunzia idadi kubwa ya turathi zetu, na yametujulisha hazina na thamani ya maktaba hiyo ambayo ni miongoni mwa maktaba kubwa hapa Iraq, iliyojaa maarifa, elimu na fikra, mwenye maktaba hiyo ni kinara wa ushia, alisoma katika shule za Najafu, Kadhimiyya na Samaraa, ni mtu aliyekusanya elimu nyingi”.

Kitabu hiki ni miongoni mwa vitabu vya kitamaduni vilivyo kusanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni sehemu ya kuongeza vitabu vya turathi katika maktaba zetu na kutoa fursa kwa wasomi ya kuandaa tafiti zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: