Haya yamethibitishwa kwenye mtandao wa Alkafeel na rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim, amesema: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ya kufungua makumbusho ya Alkafeel baada ya kufungwa kwa muda mrefu kwa sababu ya janga la maambukizi ya virusi vya Korona, tumechukua hatua za kujilinda na maambukizi kwa ajili ya kulinda usalama wa mazuwaru na watumishi wa makumbusho, tunafuata maelekezo yote yaliyotolewa na idara ya afya”.
Miongoni mwa mambo yatakayo zingatiwa ni:
- - Watu wataingia kwa utaratibu maalum wakiwa wamesimama umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu na kuhakikisha hakutokea msongamano.
- - Dawa itapulizwa wakati wote katika sehemu zote za makumbusho.
- - Kutakuwa na sehemu maalum za kupulizwa dawa mazuwaru ndani ya makumbusho.
- - Watawekwa watumishi watakao ongoza utembeaji wa mazuwaru ndani ya makumbusho, ili kuhakikisha misafara ya mazuwaru haisimami sana na kusababisha msongamano.
Kumbuka kuwa baada ya kutokea janga la maambukizi ya virusi vya Korona, makumbusho ilifungwa chini ya maelekezo ya idara ya afya, na sasa hivi baada ya kurudi harakati za mazuwaru chini ya kanuni na maelekezo ya idara ya afya, makumbusho nayo imefunguliwa, kwani huzingatiwa moja ya vituo muhimu vya mazuwaru baada ya kumaliza ibada ya ziara.