Kuhitimisha semina rasmi ya fani ya uhadhiri

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimehitimisha semina ya (fani rasmi ya uhadhiri) iliyo walenga watumishi wa idara za Atabatu tukufu na hospitali ya rufaa Alkafeel, iliyo fanywa kwa lengo la kuongeza uwezo wa watumishi hao.

Dokta Muhammad Jaabir rais wa kitengo hicho ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinatekeleza majukumu yake kwa kufuata mpango kazi wa muda mrefu, katika kuwajengea uwezo watumishi na kuboresha utendaji wao, nayo ni sehemu ya ratiba inayo lenga kuboresha rasilimali-watu na kujikita katika maendeleo endelevu”.

Akaongeza kuwa: “Kufuatia mfululizo wa semina za (fani rasmi ya uhadhiri) ambayo wameshiriki watumishi wa idara za Ataba tukufu na wahudumu wa hospitali ya rufaa Alkafeel pamoja na baadhi ya watumishi wa kitengo hiki”.

Mkufunzi wa semina hiyo bwana Ahmadi Dakhal amesema kuwa: “Katika semina hii tumeeleza kwa urefu namna ya kutoa muhadhara na aina zake, sawa uwe Mhadhara wa ndani au wa nje, tumefundisha pia namna ya kutumia mitandao ya kisasa katika kutoa mihadhara, sambamba na kupanga maudhui wakati wa kuratibu maktaba kwa mfumo mpya wa uongozi wa maktaba, pamoja na maeneo mengine muhimu ya kuamiliana na vitu vya pembezoni”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: