Mada zinaendelea kutolewa kwa lugha ya kiengereza katika kongamano la kielimu Al-Ameed awamu ya tano

Maoni katika picha
Jioni ya siku ya Ijumaa mwezi (5 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na tarehe (23 Oktoba 2020m) kwa siku ya pili mfululizo kikao cha pili cha mihadhara ya kiengereza kinaendelea, chini ya ratiba ya kongamano la kimataifa na kielimu Al-Ameed awamu ya tano, linalo simamiwa na kituo cha kimataifa cha elimu na utafiti Al-Ameed chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, linalo endelea hivi sasa chini ya kauli mbiu isemayo (Tunakutaka katika ukumbi wa Al-Ameed kwa maendeleo) kwa anuani ya (Selebasi za masomo na tafiti.. asili, uhalili na uadaaji wake).

Kikao kimeongozwa na Profesa Haidari Ghazi Mussawiy, wameshiriki watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq, baada ya kuwakaribisha na kuwatambulisha, walianza kuwasilisha tafiti zao chini ya ratiba waliyo pangiwa kwa mujibu wa mada za kongamano, na ilikuwa kama ifuatavyo:

Mada ya kwanza: (Utafiti kuhusu Shia katika mtazamo wa kielimu wa Uingereza) kwa kutoa baadhi ya mifano, imetolewa na profesa Oliva Shard Burud kutoka chuo kikuu cha Birimighiham Uingereza.

Mada ya pili: (Mfano wa wazi kwa familia zinazo saidia kuendeleza selebasi) imetolewa na Dokta Maryam Ithaar kutoka Iraq.

Mada ya tatu: (Misingi ya kisasa kuelekea selebasi ya wazi) imetolewa na Dokta Walidi Ridhwa Jawaad/ baadhi ya mifano kutoka Iraq.

Mada ya nne: (Uasili wa selebasi katika upande wa thamani) imetolewa na Dokta Wafaa Swahibu Mahadi kutoka Iraq.

Baada ya kumaliza mada hizo, ambazo tunatarajia kitafuata kikao kingine jioni ya kesho, kulikuwa na majadiliano pamoja na maoni ya washiriki.

Kumbuka kuwa kongamano litadumu kwa muda wa siku tatu na kutakuwa na mada zitakazo wasilishwa kwa lugha ya kiengereza kutoka kwa wahadhiri wa ndani na nje ya Iraq, kupitia link ifuatayo:

https://us02web.zoom.us/j/3740873005
Meeting ID: 374 087 3005
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: