Kupangilia warsha ya kielimu kuhusu selebasi ya kufundishia na tafiti pamoja na athari zake katika kumjenga mtu

Maoni katika picha
Kituo cha utafiti cha kimataifa Al-Ameed chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye ratiba ya siku ya pili ya kongamano la kielimu awamu ya tano linalo endelea sasa hivi kupitia jukwaa la (zoom).

Warsha imeongozwa na Dokta Alaa Jabiri Mussawi na jumla ya mada tano zimewasilishwa kama ifuatavyo:

  • - Dokta Hatim Jaasim Azizi mada isemayo (Namna ya kuwasilisha selebasi ya masomo katika mazingira ya janga la Korona na athari zake kinafsi).
  • - Dokta Swalehe Mahadi Zaamiliy mada isemayo (kuboresha selebasi ya masomo na changamoto za mustakbali).
  • - Ustadh Ahmadi Abdulhussein Azirujawi mada isemayo (selebasi ya masomo baina ya mazingira na uhalisia).
  • - Dokta Muhammad Muhsin Jabiri mada isemayo (mfano uliopendekezwa katika athari za selebasi na maendeleo binafsi).
  • - Dokta Muhammad Kadhim Jadhiliy mada isemayo (selebasi iliyo fichika na athari zake kwa mwanafunzi).

Mada hizo zimejadiliwa katika warsha pamoja na mada zingine zinazo fungamana na mambo hayo, ikiwa ni pamoja na nafasi ya selebasi za masomo na athari yake katika kujenga watu kitamaduni, kifikra na kimaadili, na kuzifanya ziweze kuchukua nafasi yake kwenye jamii, kwa kuonyesha athari kwa mwanafunzi, kwani inatakiwa kuathiri mwenendo, utamaduni na fikra zake sambamba na kuangalia hatari inayo weza kutokea katika makuzi, hivyo ni muhimu sana kuiangalia kwa mazingatio makubwa.

Washiriki wa warsha wamechangia mada vizuri na kutoa maoni yao, aidha wameuliza maswali yaliyo jibiwa na watoa mada pamoja na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika.

Tambua kuwa kongamano litakuwa na vikao vinne na watafiti kutoka ndani na nje ya Iraq watawasilisha mada zao kupitia link ifuatayo:

https://us02web.zoom.us/j/3740873005
Meeting ID: 374 087 3005
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: