Kuanza kazi za awali katika ujengaji wa sakafu ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza kazi wa ujenzi wa sakafu ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inahusisha uwanja unaoelekea kwenye haram, ambao ulijengwa mwaka huu, hadi unapokutana na haram tukufu.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaighi amesema kuwa: “Hakika mlango wa Kibla ndio mlango mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kumaliza kuutengeneza na kuufanyia upanuzi sehemu ya mbele na kuweka mapambo na nakshi za kiislamu kwenye paa ya mlango na ukuta wake, sasa tumeanza kujenga sakafu yake, tayali tumeanza kuondoa tabaka la juu lililojengwa kwa muda, halafu tutachukua vipimo maalum vinavyo endana na muinuko wa ardhi, uwanja pamoja na milango yake, halafu tutaweka marumaru nzuri na imara”.

Kumbuka kuwa utengenezaji wa eneo la mlango huu ni sehemu ya mradi mkubwa wa upanuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao umeongeza ukubwa wa milango tofauti na zamani, na kuongeza nakshi na mapambo ya kiislamu kulingana na nafasi ya kila mlango, ili iweze kuingiza idadi kubwa ya mazuwaru na mawakibu Husseiniyya ndani ya Ataba tukufu, milango hiyo imesanifiwa na kutengenezwa kupitia shirika la ujenzi la ardhi tukufu na kusimamiwa moja kwa moja na kitengo cha usimamizi wa miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuzingatia umuhimu wa milango hiyo na kuhakikisha utengenezaji unafanywa kwa umakini na ufanisi mkubwa, hivyo kazi hiyo ilikuwa inahitaji muda mrefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: