Kituo cha turathi za Basra kinaangazia turathi za Allamah Shekh Kadhim Hilfiy (q.s).

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa kitabu cha (Mwanga unao angazia uhai wa Allamah Mhakiki Shahidi Shekh Kadhim Hilfiy) kwa kalam ya Muheshimiwa Shekh Falahu Hilfi, kimepitiwa na kuhakikiwa na kituo cha turathi za Basra, kitabu jumla kinakurasa (356).

Makamo kiongozi mkuu wa kituo cha turathi za Basra Mheshimiwa Shekh Yasini Yusufu amesema: “Mwenyezi Mungu mtukufu ameupenda mji wa Basra kwa kuupa neema nyingi na ameupamba kwa sifa nzuri, ikiwemo wingi wa watu walio amini yaliyo ahidiwa na Mwenyezi Mungu kwao tangu ulipo anzishwa mji huo hadi sasa, hatuwezi kuwasahau mashahidi wetu watukufu waliokuwa taa lililoangazia watu huru waliotekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ni wajibu wetu kuhifadhi turathi za watu hao wema, na kuhuisha kumbukumbu zao, sio kwa kwa ajili ya kuwashukuru peke yake, bali kila mmoja kati yao alikua shule ambayo tunapaswa kuilinda na kunufaika nayo”.

Akafafanua kuwa: “Kitabu kimeangazia uhai wa mmoja wa watu hao, nae ni Muheshimiwa Allamah Shahidi Saidi Shekh Kadhim Hilfiy, alikuwa kinara wa Akhlaq kabla ya kuwa kinara wa elimu, alikuwa mpambanaji mwenye msimamo imara mbele wa Twaghuti kabla ya kuwa mpambanaji wa uandishi na utunzi wa vitabu, alikuwa mwanajeshi mtiifu wa Marjaa, alimtumikia Mwenyezi Mungu mtukufu hadi akauwawa shahidi mikonini mwa watumishi waovu wa Sadamu, tumekusanya taarifa zinazo muhusu kwa kufuata utaratibu unao faa, kisha tumepanga faharasi inayo endana na mada za kitabu”.

Tambua kuwa unaweza kusoma kitabu hicho pamoja na vitabu vingine vinavyo chapishwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kupitia toghuti ifuatayo www.mk.iq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: