Maukibu za Karbala zinaomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) katika malalo yake takatifu huko Samaraa

Maoni katika picha
Atabatu Askariyya tukufu imeshuhudia idadi kubwa ya mawakibu za kuomboleza kifo cha Imamu Askariy (a.s), miongoni mwa mawakibu zilizo shuhudiwa ni mawakibu za watu wa Karbala, kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kilicho chini yao.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyo tolewa na rais wa kitengo hicho bwana Riyadhi Ni’mah Salman, akaongeza kuwa: “Hakika Ataba mbili tukufu zimeandaa gari zenye ukubwa tofauti kwa ajili ya kubeba mawakibu na waombolezaji kutoka Karbala hadi Atabatu Askariyya katika mji wa Samaraa”.

Akaendelea kusema: “Maukibu nyingi na vikundi vya Husseiniyya vimeshiriki kuomboleza, baada ya matembezi wamefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram ya Maimamu wawili Askariyyani (a.s), na kusoma kaswida na tenzi za kuomboleza ziliazo amsha hisia za huzuni katika kuwapa pole Ahlulbait (a.s) kutokana na msiba huu”.

Kumbuka kuwa maukibu za kuomboleza ni utamaduni ulio zoweleka kufanywa kila mwaka na watu wa Karbala katika kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), nazo ni miongoni mwa mawakibu ambazo husaidiwa na Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, na huandaa mazingira ya uombolezaji, hususan zinazo fanywa nje ya mkoa kwenye matukio tofauti, likiwemo tukio hili la kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: