Mawakibu za kuomboleza zinamiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuhuisha na kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s), Ataba mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) tangu mapema leo asubuhi, zimeshuhudia mawakibu za waombolezaji zikija kuomboleza msiba huu na kumpa pole Imamu wa zama (a.f).

Hakika mawakibu za kuomboleza kifo cha Imamu yeyote huanza mapema, ikiwa ni pamoja na kifo cha Imamu Askariy (a.s), huu ndio utamaduni wa tangu zamani, watumishi wa malalo mbili takatifu kupitia kitengo cha mawakibu na maadhimisho huratibu matembezi ya waombolezaji hao kwa kuweka ratiba maalum.

Kumbuka kuwa waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kila sehemu ya dunia huomboleza msiba huu na kumpa pole Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) kwa kifo cha baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s), aliye uwawa kishahidi na mtu muovu zaidi, alipewa sumu kali na Mu’tamadi Abbasiy, akaugua siku kadhaa baada ya kula sumu hiyo, akafariki (a.s) akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, alikufa mwezi nane Rabiul-Awwal mwaka wa (260h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: