Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya imeanza semina ya maarifa ya Quráni tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kutoa semina za maarifa ya Quráni pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi.

Siku ya kwanza ya semina hiyo mkufunzi alikuwa ni Shekh Hamza Fatalawi, ameanza kwa kuongea historia tukufu ya Mtume (s.a.w.w), na umuhimu wa maarifa ya kitabu kitakatifu kilicho husiwa na Mtume pamoja na Ahlulbait wake (a.s), mwisho wa mada yake washiriki walipata fursa ya kujadiliana.

Semina hii ni sehemu ya utamaduni wa kila mwaka unaolenga kuimarisha utamaduni wa kufuata mafundisho ya Quráni tukufu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni chini ya kitengo cha maarifha ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imezowea kufanya harakati mbalimbali za Quráni kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: