Zawadi ya Qamaru ya turathi za kiislamu kimataifa yaahirishwa hadi mwakani

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuahirisha zawadi ya Qamaru ya turathi za kiislamu hadi mwaka kesho (2021), badala ya mwaka huu, kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, muda utapangwa wakati ukifika.

Zawadi ya Alqamaru ni ya kimataifa na inalenga kuenzi utamaduni na turathi za kiislamu, kama ifuatavyo:

  • 1- Kuinua kiwango cha kuhakiki, kuandika, kuandaa faharasi na kutafsiri turathi, kwa kufuata misingi ya kielimu.
  • 2- Kushajihisha watu na taasisi kulinda turathi za kiislamu na kuzitangaza.
  • 3- Kusaidia wadau wa turathi na kulinda utambulisho halisi wa kiislamu.
  • 4- Kuingiza kwenye maktaba za kiislamu mambo muhimu ya turathi za kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: