Hatua za mwisho za kuupokea mwaka mpya wa masomo

Maoni katika picha
Shule za Al-Ameed zimekamilisha maandalizi ya kuingia mwaka mpya wa masomo, maandalizi hayo yamehusisha ukarabati wa majengo ya shule pamoja na kuweka vifaa vya kujikinga na maambukizi.

Rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Ahmadi Kaabi amesema kuwa: “Miongoni mwa kazi za maandalizi, idara ya utumishi na vifaa katika kitengo cha malezi na elimu ya juu pamoja na idara ya shule za Al-Ameed, zinafanya ukarabati katika majengo ya shule zake, ili kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi, kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, wamefunga mitambo ya kupuliza dawa katika maeneo ya shule hizo”.

Akaongeza kuwa: “Ukarabati huo umetanguliwa na kuongeza madarasa pamoja na kupanua vyumba za madarasa kwenye baadhi za shule, ikafuata kazi ya kusafisha bustani na viwanja vya shule”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: