Chuo kikuu cha Alkafeel na Al-Ain zinaangalia namna ya kushirikiana

Maoni katika picha
Ugeni kutoka chuo kikuu cha Al-Ain katika mkoa wa Dhiqaar ukiongozwa na rais wa chuo hicho Dokta Shafiqu Shaakir Maula, umetembelea chuo kikuu cha Alkafeel kilicho chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya na kupokelewa na rais wa chuo hicho Dokta Nuuris Dahani.

Wageni wametembelea kumbi za chuo na maabara pamoja na sehemu zingine za chuo, na wakaangalia mfumo wa kisasa wa elimu unaotumiwa na chuo hicho pamoja na mambo mengine.

Mwishoni mwa ziara hiyo Maula akasema: “Tumefanya ziara hii kwa ajili ya kutambua vitu vinavyo milikiwa na chuo, majengo, maktaba na kumbi za madarasa, na kuangalia namna ya kushirikiana katika sekta ya elimu na selebasi za masomo, sambamba na kuangalia namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kubadilishana walimu na kutembeleana mara kwa mara, na kufanya makongamano ya pamoja ya fani mbalimbali zinazo fundishwa na vyuo vyetu”.

Akasisitiza kuwa: “Chuo kikuu cha Alkafeel kinamaendeleo makubwa na tunaweza kusema kuwa kinalingana na vyuo vya kimataifa kwa kila sifa”.

Naye mkuu wa chuo cha Alkafeel Dokta Nuuris Dahani akasema kuwa: “Tunatarajia ziara kama hizi ziimarishe ushirikiano wa kielimu baina ya vyuo vyetu, na kuongeza utafiti utakao saidia kutatua changamoto za kielimu na kuleta maendelea katika taifa letu kipenzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: