Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinashindikiza wapiganaji wake watatu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) asubuhi ya Jumanne (16 Rabiul-Awwal 1442h) sawa na tarehe (3 Novemba 2020m) imeshindikiza wapiganaji wake watatu waliopata shahada katika ajali iliyotokea wakati wakitekeleza majukumu yao katika mji wa Najafu.

Wamefanyiwa ziara na kusomewa dua ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kumalizia katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: