Rais wa chuo cha Basra katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu amesifu msaada wa serikali kielimu

Maoni katika picha
Rais wa chuo kikuu cha Basra Dokta Saadi Shahin Hamadi ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kufanya ibada ya ziara amekutana na mjumbe wa kamati kuu Ustadh Jawadi Hasanawi.

Ziara hii ni sehemu ya ratiba ya kongamano la Multaqa-Thaqafi ya kupokea wageni kutoka katika vyuo na shule za kisekula, linalo simamiwa na idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ugeni huo umehusisha viongozi wa vyuo vikuu na wakufunzi.

Wamejadili mambo mengi katika mazungumzo yao, ikiwa ni pamoja na mambo yanayo husu masomo ya kisekula, na mkakati wa Atabatu Abbasiyya katika sekta hiyo, ugeni huo umeangalia mambo yanayo fanywa na chuo pamoja na kuonyesha umuhimu wa kukuza uhusiano na taasisi za Ataba tukufu, hilo ndio jambo la kwanza katika makubaliano ya kushirikiana baina yao na chuo kikuu cha Al-Ameed, kuwe na ushirikiano wa kubadilishana maarifa na mambo yenye faida na pande zote mbili.

Rais wa chuo amesifu mapokezi mazuri waliyo pewa na ukarimu walio fanyiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na ufadhili wa Ataba katika mambo mbalimbali ya kielimu sambamba na kupokea wanafunzi wa fani tofauti, akasema kuwa mkutano huo umekuwa na faida kubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: