Ugeni kutoka chuo kikuu cha Basra unahitimisha ziara yake katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutembelea miradi na vitengo vyake

Maoni katika picha
Ugeni wa chuo kikuu cha Basra umehitimisha ziara katika Atabatu Abbasiyya ambayo ilikua ndani ya ratiba ya Multaqa kwa kupokea wageni kutoka vyuo vikuu. Linalo andaliwa na idara ya uhusiano wa vyuo vikuu na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya na kutembelea miradi ya Ataba na vitengo vyake.

Wametembelea vitengo kadhaa vya Atabatu Abbasiyya tukufu na miradi yake, na kuangalia kazi kubwa inayofanywa ya kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru na jamii kwa ujumla, wakahitimisha ziara yao kwa kukutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajumbe wa kamati kuu pamoja na marais wa vitengo.

Mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi amesema kuwa: “Ugeni wa Basra ulihusisha rais wa chuo kikuu na viongozi wa vitivo vya chuo pamoja na wakufunzi, ziara hii ipo katika utaratibu aliowekwa na kitengo cha uhusiano kupitia idara ya mawasiliano na vyuo vikuu, yenye jukumu la kuimarisha ushirikiano kati ya Ataba na taasisi za kielimu, kwa kubadilishana maarifa na kurudisha Imani ya uwezo wa kiakili wa raia wa Iraq”.

Akaongeza kuwa: “Zimeundwa kamati za pamoja kati ya Atabatu Abbasiyya na chuo kikuu cha Basra, kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa vipengele walivyo kubaliana pande hizo mbili, vinavyo lenga kushirikiana katika mambo ya kielimu na kubadilishana maarifa”.

Kumbuka kuwa ziara imedumu kwa muda wa siku mbili, pia kulikua na muhadhara uliotolewa na kiongozi wa kituo cha utamaduni na habari za kimataifa chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Jaasim Saidi, aliyetambulisha miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu na mafanikio yaliyo patikana, aidha ugeni huo umetembelea Atabatu Husseiniyya na kukutana na viongozi wa Ataba hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: